Sunday, April 12

SIKU NJEMA YA UFUFUO!

Warumi 8:1

Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

Hata wakati mbaya kabisa wa giza katika historia, Mungu alikuwa kazini, ili kuhakikisha mwanadamu anapata wokovu.

Pale Msalabani palikuwa na mabadilishano ya Kiungu ambapo hukumu ya kifo tuliyostahili ilibadilishwa kwa rehema yake na tukapewa uzima wa milele.

Hii ndiyo sababu tunasheherekea Ufufuo wa Yesu Kristo.

Alikamatwa

Aliteswa

Alipigwa

Alidharauliwa

Alivuliwa nguo zote

Alidhalilishwa

Alisemwa vibaya

Alipingwa

Alihukumiwa pasipo kosa

Alitemewa mate

Alichekwa

Alifanyiwa ukatili wa kutisha

Alifyonywa

Alitikisiwa kichwa

Alikodolewa macho

Alizuiliwa mikono na miguu

Aliharibiwa

Alisulubiwa pamoja na wanyang'anyi

Alichomwa mkuki ubavuni

Alisema Mungu wangu mbona umeniacha

Hakuweza tena kumwita Mungu, BABA kama alivyozoea

Kwa sababu alifanyika dhambi ili sisi tuhesabiwe haki

ALISEMA IMEKWISHA

Alimkabidhi Mungu Roho yake

Alizikwa kaburini

Alifungiwa na jiwe kubwa lenye muhuri

Alilindwa kuhakikisha hafufuki

Alishuka kuzimu

SIKU YA TATU AKAFUFUKA TOKA KWA WAFU

Jiwe halikumzuia kutoka kaburini

Yote hayo yalifanyika ili mimi na wewe tupate uzima wa milele

Ndugu unayesoma ujumbe huu wa Pasaka njema ya Ufufuo, kama hujampa Yesu maisha yako, basi nakuomba useme maneno haya hapa chini ili ufanyike Mwana wa Mungu.

Mungu wangu ninamkiri Yesu kwa kinywa changu ya kuwa ni Bwana, na ninaamini moyoni mwangu ya kuwa wewe Mungu ulimfufua katika wafu, kwa hiyo nimeokoka.

Kwa maana kwa moyo nimeamini hata kupata haki, na kwa kinywa nimekiri hata kupata wokovu.

Asante Yesu kwa Neema yako.

Asante Mungu kwa pendo lako.

Asante Roho Mtakatifu kwa ushirika wako.

Basi ndugu mpendwa umekuwa mwana wa Mungu, hongera sana kwa muujiza huu mkubwa kabisa wa kuokoka.

Yohana 1:12

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

Ukiwa unahitaji msaada wa jinsi ya kukua kiroho tuwasiliane kwa namba hii 0754809462.

Frank Riessen

No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.