Wednesday, July 1

JINSI YA KUOMBEA KANISA

I. OMBEA KANISA LAKO 
A. Omba mara kwa mara kwa ajili ya Kanisa – Kuombea Kanisa mara kwa mara itasaidia mioyo yetu kujiunganisha na Kanisa na kuhisi kile ambacho Mungu anahisi kwa Kanisa katika eneo letu.

B. Ona Kanisa kama suluhisho la Mungu kwa mji wetu – Maombi yote katika Agano Jipya yameelekezwa maalumu kwa ajili ya Kanisa. Hii haimaanishi kwamba tusiombee waliopotea, ila in maana Mungu analiona Kanisa kama jawabu la mambo mbalimbali katika mji wetu.

1. Kuombea Kanisa ni kuombea waliopotea kwa sababu Kanisa lenye nguvu na imara katika mji wako litapelekea kuokolewa kwa waliopotea na kutoa majibu ya mambo mengine ya giza katika mji. Mungu anatamani kutoa majibu ya uovu, giza na dhambi kupitia Kanisa lenye nguvu na imara. 

2. Usiombee kusanyiko lako tu lakini pia omba kwa ajili ya Kanisa katika mji wako. Ingawaje Kanisa lina kusanyiko la mtu mmoja mmoja na makundi tofauti, mara zote tunahitaji kuombea moyo wa Bwana kwa Kanisa zima katika mji wetu. Mungu hatamani kutembelea kusanyiko moja tu bali anatamani kuachia nguvu kwa Kanisa zima katika mji mzima.

C. Muombe Roho Mtakatifu kwa ajili ya ufunuo – Kadri unavyoombea Kanisa kwenye eneo lako, muombe Roho Mtakatifu anachokihisi kuhusiana na Kanisa katika eneo lako. Sikiliza na omba katika ufunuo Bwana aliokupa. Lengo, kwa wakati si tu kuombea Kanisa katika njia ya kutengana bali kuanza kuhisi Moyo wa Bwana kwa Kanisa katika eneo lako na kukubaliana na vitu vilivyomo katika moyo wake.

D. Omba maombi chanya kwa Kanisa – Daima omba maombi chanya kwa ajili ya Kanisa na waumini. Ukiwa chini ya mzigo, usiombe kuhusiana na maombi hasi ya mzigo ulionao, lakini omba kwa ajili ya kupata mambo chanya.
1.  Tukiomba maombi hasi, roho zetu zinakuwa hasi. Wakati kuna matatizo ya kweli katika Kanisa, omba kwa ajili ya vitu vizuri ambavyo Mungu anavitamani ambavyo vitaweka mioyo hai wakati tunaombea Kanisa. Katika mikutano ya maombi, ni vizuri sana kuomba kwa njia chanya. Maombi hasi kwa haraka sana yatafanya mikutano yetu ya maombi isiwe ya kufurahisha na inachangia pia roho ya ugomvi katika Kanisa kwenye mji wetu.
2.  Tukiomba maombi chanya ianatusaidia kuzuia roho ya hukumu. Wakati Mungu anaachilia mzigo wake kwetu kama sehemu ya maombi, tunataka daima kuzuia roho ya hukumu kwa waamini wengine. Mara nyingi tukiomba maombi hasi tunaweza kuasili roho ya kujiona bora juu ya waamini ambao tunahisi wapo katika maelewano na tunataka kuepuka hii roho.
E. Tumia maombi ya Kitume – Unapoanza kuomba kwa ajili ya kanisa katika mji wako, tumia maombi ya Kitume kutoka Agano Jipya. Kila maombi kwenye Agano Jipya ni maalumu kwa ajili ya eneo au mji fulani. Haya maombi yanatupa lugha ambayo tunaweza kuomba kwa ajili ya Kanisa. Kama unahisi mzigo kwa ajili ya Kanisa kwenye eneo lako, ombea upande chanya wa mzigo (hivi ni kusema: unataka Mungu afanye nini kwa Kanisa) na tafuta maombi ya Kitume kuhusiana na hayo maudhui. Kitambo kidogo, kuomba maombi haya itakupa lugha ya Kibilia na mfano wa Kibiblia kwa ajili ya kuombea Kanisa.  

II. MAOMBI MUHIMU YA KITUME NA AHADI ZA KINABII

1. OMBA UFUNUO WA UZURI WA YESU ILI TUTEMBEE KATIKA WITO NA HATIMA YA NGUVU YA MUNGU.
17 Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye (kumfahamu);
 18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake (uhakika/kweli ya wito wa Mungu kwa maisha yetu) jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu (hatima yetu kama urithi wa Yesu) jinsi ulivyo;
 19 na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; (Efe. 1:17-19) 

2. OMBA KUPOKEA NGUVU YA ROHO KWAMBA UWEPO WA YESU UJIDHIHIRISHE KWETU ILI TULIJUE PENDO LA MUNGU.
16 awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.
 17 Kristo akae (uwepo wake ukae) mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina (mzizi) na msingi katika upendo;
 18 ili mpate kufahamu (kujua) pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina;
 19 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu. (Efe. 3:16-19) 

3. MAOMBI ILI UPENDO WA MUNGU UZIDI KUWA MWINGI KWETUKWA UFAHAMU WA MUNGU KUTULETEA HAKI KATIKA MAISHA YETU. 
9 Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;
 10 mpate kuyakubali (kufurahia) yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi (bila kupinga), bila kosa, mpaka siku ya Kristo;
 11 hali mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu. (Fil.1:9-11)
4. MAOMBI YA KUJUA MAPENZI YA MUNGU, ILI KUZAA MATUNDA KATIKA HUDUMA NA KUIMARISHWA/KUWEZESHWA NA UKARIBU WA MUNGU. 
9 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;
 10 mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;
 11 mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha; (Kol. 1:9-11)

5. MAOMBI KWA AJILI YA UMOJA KATIKA KANISA NA ILI MJAZWE FURAHA KUU, AMANI NA TUMAINI (UHAKIKA/KUJIAMINI)
5 Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu;
 6 ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. (Rum. 15:5-6, 13)

6. KUTAJIRISHWA NA KARAMA ZOTE ZA ROHO IKIWEMO MAHUBIRI YENYE NGUVU NA UFUNUO WA KINABII. 
5 kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, (kupakwa mafuta ya kuhubiri/kuimba) na maarifa yote (maarifa ya kinabii);
 6 kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu;
 7 hata hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;
 8 ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. (1 Kor. 1:5-8)

7. KUOMBA KUACHILIWA KWA NEEMA YA KULILETA KANISA KATIKA UKOMAVU HASWA WA KUZIDI KATIKA UPENDO NA UTAKATIFU
10 usiku na mchana tunapoomba kwa juhudi tupate (Mungu aachilie Roho yake na neema) kuwaona nyuso zenu, na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu?
12 Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;
 13 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote. (1 Thes. 3:10, 12-13)

8. OMBA ILI USTAHILI (UTAYARISHWE AU UFANYWE KUKOMAA KIROHO) KUTEMBEA KATIKA UKAMILIFU WA HATIMA YETU KWA MUNGU.
11 Kwa hiyo twawaombea ninyi sikuzote, ili Mungu wetu awahesabu (kututayarisha kwa ajili) kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema (mipango kwa ajili yetu) na kila kazi ya imani kwa nguvu;
 12 jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo. (2 Thes. 1:11-12)

9. OMBA KWAMBA NENO LIONGEZE USHAWISHI WAKE ( UFANISI) KWENYE MJI KADIRI MUNGU ANAVYOACHILIA NGUVU ZAKE KWENYE NENO
1 Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, (kuongeza kasi ya ushawishi wake) na kutukuzwa (likithibitishwa kwa nguvu ya kitume na miujiza) vile vile kama ilivyo kwenu;
 2 tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.
 3 Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.
 4 Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza, tena kwamba mtayafanya.
 5 Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi (uvumilivu na usatahimilivu) ya Kristo. (2 Thes. 3:1-5)

10. OMBA KWA AJILI YA KUWEKEWA UJASIRI (KUIMBA NA KUTAMKA NENO) KWA KUACHILIA UPONYAJI, ISHARA NA MAAJABU
29 Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote,
 30 ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
 31 Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. (Mdo 4:29-31)

11. KUACHILIWA KWA BARAKA ZA MUNGU ZILIZOPEWA NGUVU KWA WOTE WANAONGOJEA (WANAOOMBA) UPENYO
49 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu. (Luk. 24:49).
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. (Mdo 1:8)

12. OMBA KWAMBA MUNGU ATOE BIDII/JUHUDI ZAKE KWA WATU WAKE NA UDHIHIRISHO WA UWEPO WAKE UTINGISHE/UTETEMESHE WOTE WANAOMPINGA
15 Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi (udhihirisho) wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
 16 Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.
1 Laiti ungepasua mbingu, na kushuka (kudhihirisha nguvu zako), ili milima (vikwazo) iteteme mbele zako;
 2 kama vile moto uchomapo vichaka, na moto uchemshapo maji; ili kuwajulisha adui zako jina lako, (dhambi, magonjwa, shetani) mataifa wakatetemeke mbele zako!
 3 Ulipofanya mambo ya kutisha tusiyoyatazamia, ulishuka, milima ikatetema mbele zako.
 4 Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye.
 5 Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika mambo haya muda mwingi; nasi, je! Tutaokolewa?
 6 Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.
 7 Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu. (Isa. 63:15-16; 64:1-7)

13. MAOMBI KWA AJILI YA KUTOLEWA KWA AHADI YA MUNGU YA KUMWAGWA KWA ROHO WAKE NA KUPATA NDOTO, MAONO NA UNABII
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
 18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.
 19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi.
 20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.
 21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. (Mdo 2:17-21)

14. MAOMBI KWA AJILI YA ISRAELI KUOKOLEWA NA KUTOLEWA KWA UPAKO WA KINABII, MIUJIZA NA HAKI
1 Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe. (Rum. 10:1)
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasi yake.
 27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao. (Rum. 11:26-27)
1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza (au kuwa kimya: kutolewa roho ya unabii), na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia (au sitakuwa asiyetenda: kutolewa nguvu), hata haki (katika masuala yote ya moyo) yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo (huduma kwa wengine). (Isa. 62:1)

Maombi Halisi ya Agano la Kale kwa ajili ya Israeli 

(Isa. 63:15-64:12; Dan. 9:4-19; Mik. 7:7-20; Hab. 3:2-19; Ezra 9:5-15; Neh. 1:4-11; 9:5-38; Zab. 44; 45:3-5; 65; 67; 79; 80; 83; 85; 86; 90:13-17; 102:12-22; 110:1-5, 122:6-7; 132:11 

Ahadi za kinabii za Agano la Kale za kuomba juu ya Israeli (ukweli huu pia unaweza kuombwa kwa Kanisa): 
Kumb. 4:27-31; 30:1-10; 31:29; 33:26-29; Isa. 11:10-16; 29:14, 17-24; 30:18-33; 32:15-19; 33:2-6, 17; 35:1-10; 42:10-17; 43:1-7; 44:1-5; 45:17, 22-25; 51:3-11; 54:1-17; 56:6-8; 59:19-21; 60:1-62:12; 66:7-14; Jer. 3:14-20; 16:14-21; 31:1-14; 32:16-23; 32:37-42; 33:6-26; 50:4-5; 50:19-20, 34; Ezek. 11:17-20; 16:60-63; 20:33-44; 34:11-31; 37:1-28; Hos. 2:14-23; 3:5; 5:15-6:3, 11; 14:1-8; Yoel 2:28-32; 3:17-20; Zef. 3:8-20; Hag. 2:6-9, 21-22; Zak. 8:2-8; 12:10-13:6; Mal. 4:1-6.



No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.