Tuesday, February 11

MSAFARA WA UZIMA UNAPOKUTANA NA MSAFARA WA MAUTI

Luka 7:12,14-15

12 Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye.

14 Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka.

15 Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake.

Pengine ni ndoa, huduma, biashara, mtoto, kazi yako ipo langoni kwa mji inaenda kuzikwa (Na ya pekee kabisa)

Usiogope maana Yesu mtoa UZIMA anakutana na huo msafara wa mauti unaokwenda kuzika maono yako.

Yesu anaiambia ndoa, huduma, biashara, elimu, kazi, mtoto wako aliyeshindikana INUKA NAKWAMBIA nayo bila kusita inainuka na Yesu anakukabidhi upya kile kilichokuwa kimekufa.

UZIMA ukikutana na mauti, mauti haiwezi kuhimili itakimbia tu.

Baki umebarikiwa mwana wa Mungu.

No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.