Monday, July 13

MAANDIKO YA UPONYAJI WA KIMWILI

Watu wengi wanaamini kwamba Mungu anaweza kuwaponya lakini hawana uhakika kama atawaponya wao. Kama huyo ni wewe, basi nakutia moyo usome kwa makini kila moja ya maandiko haya. Angalia ni kiasi gani Mungu anataka kuponya watoto wake. Hutakiwi kufanya kitu ili kupata upendo wake au mguso wa uponyaji wake, amini tu kile anasema na kufanya kile yeye anakwambia kufanya.
Anza kwa kutamka mistari hii kwa sauti. Tafakari juu ya maandiko haya. Yaamini. Hivyo ni jinsi tunavyoachia nguvu ya Mungu ya kuponya - kwa kusema neno lake na kuamini uwezo wake na utayari wake wa kuponya magonjwa yetu yote.
Zab 103:1-3 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote.

Zab 118:17 Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya Bwana.

Zab 147:3 Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao.

Mit 4:20-22 Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu. Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.

Kut 23:25 Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.

Mit 3:7-8 Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.

Jeremiah 17:14 Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.

Mat 9:20-22 Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake. Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.

3 Yoh 1:2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

Mak 16:17-18 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Mat  4:23-24 Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu. Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.

Mat 8:16-17 Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.

Yak 5:14-15 Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.

UKIRI KWA AJILI YA UPONYAJI WA KIMWILI: 
"Najua kuwa ni mapenzi ya Mungu kwa ajili yangu kuwa na afya na uzima. Nakusifu na kukushukuru Bwana kwa kuniponya magonjwa yangu yote kwa kuweka imani yangu na tumaini langu kwake. "

6 comments:

Barikiwa kwa ujumbe wako.