Kuhusu Furahini Daima


KUSUDI:

Kusudi la Huduma ya Mafundisho ya Furahini Daima nikufundisha nuru ya neno la Mungu kwa watu wote ili wafurahi katika Bwana sikuzote.

1 Wathesalonike 5:16 Furahini Daima.

MAONO:

Maono ya Huduma ya Mafundisho ya Furahini Daima nikuhakikisha watu wote wanapata maarifa ya neno la Mungu ili wafurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu.

1 Petro 1:8 Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; nakufurahishana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu.

MAHUSIANO NA HUDUMA NYINGINE:

Huduma ya Mafundisho ya Furahini Daima ipo wazi kushirikiana na huduma nyingine za Bwana Yesu Kristo za kitume, kinabii, kiinjilisti, kichungaji na kiualimu 

(Waefeso 4:11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu.) katika kufikia malengo ya Bwana Yesu Kristo ya kulipa Kanisa huduma tano.

MALENGO YA HUDUMA TANO ZA BWANA YESU KRISTO:
  1. Kuwakamilisha watakatifu.
  2. Kazi ya huduma kutendeka.
  3. Kuujenga mwili wa Kristo.
  4. Kuufikia umoja wa imani.
  5. Kumfahamu sana Mwana wa Mungu.
  6. Kuwa watu wakamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.
  7. Kuwa watu wazima kiroho.

Waefeso 4:11 -16 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, nakuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.

MWANZILISHI:

Wafilipi 1:6 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.

Sifa na utukufu ni kwa Bwana wetu wetu Yesu Kristo aliye mwanzilishi wa kazi/huduma zote njema, ambaye kwa wingi wa fadhili na neema yake ametupa hii huduma ya mafundisho. Kwa hiyo sisi Frank na Anna Riessen ni wafanyakazi pamoja na Mungu katika shamba la Mungu tukijitahidi kujionyesha kuwa tumekubaliwa na Mungu, watenda kazi wasio na sababu ya kutahayari, tukitumia kwa uhalali neno la Mungu.

1 Wakorintho 3:9 Maana sisi tu wafanyakazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.

2 Timotheo 2:15 Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.

No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.