Friday, January 24

VINASABA (DNA) YAKO NI VYA NANI?


Baada ya anguko Adam hakuweza kuzaa mtu kwa sura na mfano wa Mungu.

Ndiyo tunasema dhambi ya asili, kwa sababu tuna VINASABA (DNA) vya Adamu

Mwanzo 5:3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.

Tunahitaji kuzaliwa na Mungu ili tuwe na VINASABA (DNA) vya Mungu.

Ili uzaliwe kwa sura na mfano wa Mungu una jukumu la kumpokea Yesu kwenye maisha yako.

Yohana 1:12-13 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Tena neon la Mungu linatuambia tunazaliwa kwa mbegu isiyoharibika.

1 Petro 1:23 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.

Sasa tuna VINASABA (DNA) vya BABA yetu wa Mbinguni

Kama tu wana wa Mungu kinachotokea ni hichi hapa chini:

1 Yohana 3:2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.

No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.