Wednesday, December 11

MUNGU HUFURAHIA REHEMA

Mika 7:18
Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hashiki hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema.
Hakika Mungu ni mzuri sana. Anafurahia rehema, kiasi kwamba ungekuwa peke yako duniani bado angemtoa Yesu akufie msalabani.
Mungu hata siku moja hakuangalii wewe akuhukumu Bali anamtazama Yesu aliye fanyika dhambi, laana, aliyepigwa kwa ajili yetu.
Rehema za Mungu zilipelekea Mungu akamtoa mwanawe wa pekee ili sisi tufanyike wana wa Mungu.
Pokea REHEMA ya Mungu ni bure kabisa ni wewe kuwa tayari na kupokea.

No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.