Monday, August 19

ASUBUHI YAKO LAZIMA IJE KWA UWEZO WA MUNGU

Zaburi 30:5b

Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.

Sasa hivi nyakati ulizopo inawezekana ni za usiku. Lakini nakuhakikishia kwamba hamna usiku usiokuwa na asubuhi, lazima kutapambazuka tu.

Na tena usiku unapokuwa mzito ndiyo mapambazuko yako karibu sana.

FURAHA ipo karibu sana, asubuhi yako inakuja.

Yamkini magumu unayopitia yamegeuka matanga, sikia Neno la Bwana leo; Bwana atageuza matanga yako yawe MACHEZO.

Zaburi 30:11

Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha.

Hata kama walikuvika gunia Bwana anakuvika FURAHA.

Furahi na cheza ndani ya Kristo maana hii ni siku aliyoifanya Bwana ufurahi na kuishangilia.

Zaburi 118:24

Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA, Tutashangilia na kuifurahia.

Asubuhi inakuja usiogope maana hatukupewa roho ya woga.

2 Timotheo 1:7

Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

UKIRI:

Nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti sitaogopa mabaya maana Bwana yupo pamoja nami, gongo lake na fimbo yake vyanifariji.

Aliyeko ndani yangu ni mkuu kuliko yeye aliyeko katika dunia.

Nayeweza mambo yote katika Bwana anitiaye nguvu.

Warumi 8:37

Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.

" Nyakati za kuburudishwa zaja"

Frank Riessen.

0754809462

No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.