Tuesday, July 30

MUNGU AKULISHE

Mwanzo 47:12 Naye Yusufu akawalisha babaye na nduguze na nyumba yote ya babaye, kwa kadiri ya hesabu ya watoto wao.

Mwanzo 50:21 Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema.

Mwanzo 47:17 Wakaleta wanyama wao kwa Yusufu; Yusufu akawapa chakula badala ya farasi, na badala ya kondoo, na badala ya ng’ombe, na badala ya punda, naye akawalisha chakula badala ya wanyama wao wote mwaka ule.

Bwana Yesu asifiwe.

Mstari wetu wa ufunguzi wa somo unasema: Naye Yusufu akawalisha babaye na nduguze na nyumba yote ya babaye, kwa kadiri ya hesabu ya watoto wao.

Maana ya neno LISHA (Nourish) kwa muktadha wa Mwanzo 47:12 na Mwanzo 50:21 yana maana moja ya kutoa chakula au vitu vingine muhimu kwa ukuaji, afya, na hali nzuri.

Kwa mfano kuna watu wa makundi maalumu kama wajawazito, vichanga, watoto, wazee, wazazi, wagonjwa n.k hawa huwa wanalishwa (Nourished) kwa namna iliyofafafanuliwa hapo juu.

Na haishii kwenye chakula tu la hasha bali hata mavazi, ulinzi, makazi, jinsi ya kuongea nao inakuwa ni kwa tofauti kabisa yaani kuna umaalumu fulani hivi wanakuwa wanapewa ili waweze kuishi maisha bora.

Ndiyo tunaona hapo wakati ndugu za Yusufu wanaingia Israel aliwaambia ATAWALISHA. Ukisoma habari ya kuingia kwa wana wa Israel Misri utaona walipewa upendeleo maalumu  wa makazi.

Mwanzo 47:5, 6, 11 

5 Farao akamwambia Yusufu, akisema, Baba yako na ndugu zako wamekujia; 6 nchi ya Misri iko mbele yako, PALIPO PEMA PA NCHI UWAKALISHE baba yako na ndugu zako; na WAKAE KATIKA NCHI YA GOSHENI. Tena ukijua ya kuwa wako watu hodari miongoni mwao, uwaweke wawe wakuu wa wanyama wangu. 11 Yusufu AKAWAKALISHA babaye na nduguze, na KUWAPA MILKI KATIKA NCHI YA MISRI, katika MAHALI PAZURI PA NCHI, katika nchi ya Ramesesi, kama Farao alivyoamuru.

Angalia hayo maneno yanyotoka kinywani mwa Farao:
i. PALIPO PEMA PA NCHI
ii. UWAKALISHE
iii. WAKAE KATIKA NCHI YA GOSHENI (Gosheni inaelezewa kama ardhi nzuri zaidi nchini Misri, inayofaa kwa mazao na mifugo)

Pia angalia jinsi Yusufu anatekleza maagizo ya Farao kwenye mstari wa 11:
i. AKAWAKALISHA
ii. KUWAPA MILKI KATIKA NCHI YA MISRI
iii. MAHALI PAZURI PA NCHI

Mstari wa 11 unafunga kwa kusema ‘kama Farao alivyoamuru’

Neno la Mungu linasema kwenye  Muhubiri 8:4 Kwa kuwa neno la mfalme lina nguvu; naye ni nani awezaye kumwambia huyo, Wafanya nini?

Na pia linasema katika Ufunuo wa Yohana 5:10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

Nami nasimama katika nafasi ya Kifalme kwa mamlaka niliyopewa na Bwana Yesu Kristo nakutangazia kwamba ukae palipo pema pa nchi kwenye nchi ya Gosheni yako, huku ukimiliki mahali pazuri pa nchi katika jina la Yesu Kristo.
Mpendwa Bwana Mungu AKULISHE (kwa maana ya Mwanzo 47:12 na Mwanzo 50:21)  kiroho na kimwili.

Kiroho ulishwe mafundisho yasiyoghoshiwa na kimwili ulishwe mlo kamili, hii yote Bwana amabye ni Mchungaji wetu akafanye kwako maana amesema Yeye ndiye Mchungaji wako hautapungukiwa na kitu na katika malisho ya majani mabichi hukulaza na kando ya maji ya utulivu hukuongoza na yote hii anafanya kwa ajili ya jina lake. 

Kumbuka hii wala usisahau wana wa Israel walipokuwa Gosheni hawakununua mahitaji yoyote toka kwa Yusufu, wao walilishwa pasipo fedha wala thamani.

Neno linasema katika Isaya 55:1-2 Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani.
Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.

Ndugu yangu gharama ya maji ya uzima, chakula cha kiroho, divai na maziwa ni “NJONI”, soma hiyo mistari kwa makini utaona neno ‘’njoni’’ likirudiwa mara tatu, na hii ndiyo gharama pekee ya kulishwa na Mungu “NJONI” na “KUMSIKILIZA MUNGU KWA BIDII” 

Fanya maamuzi leo "NJOO" kanunue bila fedha wala thamani.

Fanya maamuzi leo ya “KUMSIKILIZA MUNGU KWA BIDII” ule kilicho chema na kujifurahisha nafsi yako kwa unono.
Na wakati ni sasa unaposoma ujumbe huu. 

2 Wakorintho 6:1(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)

Sasa tuwaangalie wa Misri jinsi walihudumiwa na Yusufu.

Nao walilishwa na Yusufu kwa mujibu wa mstari wa 17 hapo juu lakini lisha hii ya mstari wa 17 ni tofauti na lisha ya wana wa Israel. 

Neno LISHA (Feed) kwenye huu mstari lina maana ya kitendo cha kupewa chakula. Kwa hiyo ni chakula tu kwa ajili ya kujaza tumbo au mahitaji tu ya kimwili na kiroho yasiyokuwa na mpangilio unaoleta ubora kwenye maisha ya mtu. 

Pia Wamisri pamoja na kulishwa (Feed) kwa mtindo huu bado waliingia gharama kubwa kununua hii lishe duni tofauti na Wana wa Israel.

Katika jina la Yesu, Mungu akulishe (Nourish) tofauti na Wamisri wa leo kwa gharama ya kumwendea tu Yesu Kristo tu na kumsikiliza kwa bidii.

Bwana Yesu akukinge na mapigo yote yaliyowapata Wamisri maana wewe upo Gosheni. Haleluya, Gosheni ilikuwa na ulinzi maalumu wa Mungu. 

Bwana atakulinda na mabaya yote, atakulinda uingiapo na utokapo. 

BWANA NA AKULISHE (NOURISH) 

SOMO: MUNGU AKULISHE

Frank Riessen

0754809462.

No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.