Saturday, November 4

UTAMU WA KEKI (TOLEO LA PILI KWA USHIRIKIANO NA Dr Frank P. Seth)

"Tunajua kwamba, katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kufuatana na kusudi lake" (Warumi 8:28).
Keki ni tamu lakini utamu huo umepatikana baada ya kuchanganya vitu ambavyo ukivila vyenywe hupati ile ladha ya keki.
Kwa mfano, chumvi, mayai, sukari, unga ngano, baking soda n.k. Hivi vitu ukila hivi hivi kimoja kimoja hupati ladha nzuri ya keki, lakini vikichanganywa kitaalamu kwa uwiano maalumu na kupikwa unapata keki yenye ladha nzuri sana, ambayo ni tofauti sana na ladha ya kila kimoja kati ya viungo vyake.
Ndivyo na Mungu wetu alivyo, anatumia vitu vyote vizuri na vibaya kukupata mema.
Hayo mabaya na mazuri Mungu anayatumia kukupatia mema, sawa sawa na Warumi 8:28.
Angalia pia Ayubu alijua siri hii tangu zamani,
"9 Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe. 10 Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake" (Ayubu 2:9, 10).
Usije ukaanza KUMCHUKIA Mungu wakati anaweka pilipili na chumvi maishani mwako, hapo ndio ANAKUTENGENEZA uwe kitu BORA zaidi.
Frank P. Seth & Frank R. Makundi


No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.