Saturday, November 4

UTAMU WA KEKI (TOLEO LA KWANZA)

Warumi 8:28 [SWA]
Tunajua kwamba, katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kufuatana na kusudi lake.

Ili keki iwe tamu inabidi ichanganywe na vitu ambavyo ukivila vyenywe hupati ile ladha ya keki.
Mfano chumvi, mayai, sukari, unga ngano, baking soda n.k. Hivi vitu ukila hivi hivi hupati ladha nzuri ya keki, lakini vikichanganywa kitaalamu na kupikwa unapata keki yenye ladha.

Ndivyo na Mungu wetu alivyo, anatumia vitu vyote vizuri na vibaya kukupata mema.
Hayo mabaya na mazuri Mungu anayatumia kukupatia mema, sawa sawa na Warumi 8:28.

No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.