Thursday, July 2

KAZI ZA MIKONO YA MUNGU HAZIACHWI NA MUNGU

Zaburi 138:8 Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.
Hakika Mungu anatutea katika mambo yetu, kuna haja nyingi sana ambazo tunazo lakini kumbe tukimshirikisha/tukimtegemea Mungu huwa anatimiliza mambo yetu.
Na kwa sababu fadhili zake ni za milele, kamwe hatatuacha kama alivyoahidi kwamba;  na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari, Mat 28:20b.
Sisi ni kazi ya mikono yake, tukimwita kwa kumaanisha kama Bartimayo, atatusikia maana nguvu ya Mungu siku zote huwa inasikilizia kilio cha imani, halafu inatenda kazi katika ile imani. Ndipo Yesu husema; Enenda zako, imani yako imekuponya, Mak 10:52. Lakini je tupo tayari baada ya kuisikia hii sauti ya Yesu ya Enenda zako, imani yako imekuponya?

© Frank R.M Makundi.

No comments:

Post a Comment

Barikiwa kwa ujumbe wako.